Kwa mujibu wa kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, maelfu ya watu walikusanyika katika eneo la Uskudar, Istanbul, ili kulaani mashambulizi yanayofanywa na Israel dhidi ya Ghaza, na kufanya maandamano makubwa kwa anuani ya “Ghaza inaelekea kufa, zinduka!”
Waandamanaji walipandisha bendera za Uturuki na Palestina juu huku wakapaza sauti na kusema “Israel dhalimu itaangamizwa” na “kuzingirwa kwa Ghaza ni kitendo haramu.”
Walio shiriki walionesha mshikamano wao na watu wa Ghaza, huku wazungumzaji waliwataka Waislamu wote kulaani jinai zinazofanywa na Israel dhidi ya ubinadamu.
Maoni yako